Hatma ya Mchezaji PACOME Siku 14 Nje ya Yanga

Hatma ya Mchezaji PACOME Siku 14 Nje ya Yanga

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa siku 10 hadi 14 baada ya kuumía kifundo cha mguu (ankle sprain). Pacome aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Azam.

Kiungo huyo hakumaliza mchezo huo baada ya kuumia huku daktari wa timu hiyo, Moses Etutu akifunguka kuwa kiungo huyo ameumia kifundo cha mguu “Pacome aliumia kifundo cha mguu matarajio atakuwa nje kwa siku 10 hadi 14 maendeleo yake ni mazuri akizingatia maagizo tuliyompatia kwa kuhakikisha anapumzika kwa wakati anaweza akawahi au kuchelewa zaidi ya muda huo.”

Pacome amekosekana kwenye mchezo wa jana wa Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Stand United na atakosekana katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Fountain Gate utakaopigwa Aprili 20 mwaka huu. Baada ya hapo Yanga itakuwa na mchezo mwingine dhidi ya Namungo Mei 13 mwaka huu huenda akawa sehemu ya kikosi Mechi nyingine za Yanga zilizosalia ni pamoja na Tanzania Prisons itakaychezwa Sokoine jijini Mbeya, dhidi ya Dodoma Jiji na kisha Yanga itakuwa timu mwenyeji na mchezo dhidi ya watani wao Simba ambayo haijajulikana utachezwa lini.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/q5y8d3p
via IFTTT

Post a Comment

Previous Post Next Post